Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Idara

Idara

Uwezeshaji na Huduma

Inatoa huduma ya msaada wa ndani kama vile utawala, usimamizi wa rasilimali watu, fedha na uhasibu, vifaa, usimamizi wa ofisi na mifumo ya TEHAMA ya Wakala.

Huduma za TEHAMA

Inasimamia mipango na utekelezaji wa miradi mikuu, inahakikisha ufuasi wa viwango vya usalama mifumo na ufundi vilivyothibitishwa na utoaji wa msaada wa kiufundi, huduma kwa wateja kuhusu huduma za Serikali Mtandao kwa Wizara, Idara, wakala na Serikali za Mitaa 

Usimamizi wa TEHAMA

Inatoa huduma za ushauri wa kitaalamu kuhusu kujenga uwezo na maelekezo kwa Wizara, Idara, Wakala na Serikali za Mitaa na kuendesha upitiaji wa teknolojia ya kufuatilia na kutafuta teknolojia mpya na kuzitumia.

Uratibu Miundombinu ya TEHAMA

Inasimamia mipango, miundombinu ya Serikali Mtandao, vituo vya data na mifumo ya pamoja na usalama wa taarifa.