Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Miongozo na Viwango

Miongozo na Kanuni za Serikali Mtandao

Maelezo ya Muundo wa Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao

Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao vina lengo la kusaidia  Serikali katika utoaji wa huduma zilizothabiti  zaidi  na kutosheleza kwa wananchi na kusaidia utoaji wa huduma za TEHAMA  unaozingatia  thamani ya fedha  na kutoa muundo ambao:

  • Unasaidia  kubainisha huduma rudufu, kutumika tena na kushirikiana;
  • Unatoa msingi wa kutathmini uwekezaji wa Serikali  katika TEHAMA, na 
  • Unawezesha utoaji kwa ufanisi zaidi wa  huduma zilizo na gharama nafuu kutokana na kuwepo kwa viwango, kanuni na violezo vinavyosaidia katika kubuni na kutoa huduma za TEHAMA. 

Muundo wa Viwango na Miongozo wa Serikali Mtandao  umebuniwa kutosheleza mahitaji  ya “Usanifishaji Shughuli  Serikali Mtandao”. Kwa maana hiyo Usanifishaji  Shughuli  Serikali Mtandao umo  ndani ya “Viwango na Kanuni za Serikali Mtandao”. Rejea rasmi za hali ya juu za  Usanifishaji Shughuli  Serikali Mtandao  zipo kwenye nyaraka mama na nyaraka  zinazohusiana hutoa maelezo ya kina  kama yalivyotayarishwa na sekta na taasisi zenye Dira na Mifumo Mkakati.

  • Usanifishaji Shughuli  Serikali Mtandao  - Kanuni zinazokubalika  kimataifa  kwa utekelezaji wa uchambuzi wa Serikali Mtandao, ubunifu, mipango na utekelezaji  kwa kutumia mkabala ulio  mpana wakati wote kwa maendeleo fanisi na utekelezaji wa Mkakati wa Serikali Mtandao.  
Aina za Nyaraka

Ngazi ya Kwanza – Ni Nyaraka za Miongozo ya Serikali Mtandao zinazotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora kwa taasisi zote za Umma.  Miongozo ya Serikali Mtandao ya kisekta - kwa mfano Afya-mtandao, Elimu-mtandao, Sheria-mtandao nk. inayotolewa na Wizara iko katika kundi hili. Kuna waraka mama mmoja na nyaraka zinazohusiana zinazotoa miongozo ya Serikali ya Ngazi ya Sera kuhusu  mambo ya Serikali Mtandao.

Ngazi ya Pili – Ni nyaraka za Viwango vya Kiufundi  na Miongozo ya  Serikali Mtandao zinazotolewa na Wakala ya Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma kutoa “ Viwango vya Serikali vya aina moja kuhusu utekelezaji wa Serikali Mtandao” na kutoa “Miongozo ya kiufundi ya namna ya kutekeleza jitihada za Serikali Mtandao”. Nyaraka hizi hutumiwa zaidi na taasisi za umma wakati zinapotekeleza jitihada za Serikali Mtandao zenye maslahi kwa taifa, au zinazohitaji mawasiliano na zaidi ya taasisi moja. Nyaraka mama hutoa maelekezo rasmi na nyaraka zinazohusiana hujumuisha maoni ya kisekta na kitaasisi.

ngazi ya Tatu – Ni nyaraka za TEHAMA kwa mfano Sera, Mwongozo, Mchakato, Taratibu na kadhalika, zinazotolewa na taasisi za umma kwa matumizi yao ya ndani. (Nyaraka hizi zinajulikana kuwa ni nyaraka za TEHAMA za Taasisi tofauti na za Ngazi ya Pili zinazojulikana kuwa ni nyaraka za TEHAMA za Serikali). Nyaraka za mifano zinazotayarishwa kusaidia Taasisi za Umma kuandaa nyaraka zao za Sera za TEHAMA au miongozo, pia hujulikana kuwa ni nyaraka za Ngazi ya Tatu.