Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Udhibiti wa Viwango

Udhibiti wa Viwango

2015-11-09

Wakala imeandaa Miongozo inayotoa maelekezo na ufafanuzi wa taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika utekelezaji wa jitihada mbalimbali zinazohusu TEHAMA katika taasisi za umma. Miongozo iliyokwishatolewa na inatumika kwenye taasisi za Serikali ni pamoja na Orodha Hakiki ya Miradi ya TEHAMA Serikalini (Government ICT Projects Review Checklist), Vigezo vya Kuhakiki Miradi ya TEHAMA Serikalini (Government ICT Projects Review Criteria), Taratibu za Kuhakiki Miradi ya TEHAMA Serikalini (Government ICT Projects Review Procedures) na  Mwongozo wa Kusimamia Miradi ya TEHAMA Serikalini (ICT Project Management Guideline).

Pia, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuandaa Miongozo na Viwango vya Serikali Mtandao (e-Government Standards and Guidelines) inayojumuisha miongozo yote inayotumika kusimamia TEHAMA Serikalini.

Aidha, Wakala imetengeneza mfumo wa Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA Serikalini unaopokea na kutunza taarifa za miradi ya TEHAMA iliyopo na inayotarajiwa kuanzishwa Serikalini. Lengo la mfumo huu ni kuhakikisha kuwa uratibu na usimamizi wa miradi ya TEHAMA Serikalini unafanyika kwa ufanisi.