Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Usimamizi wa TEHAMA

Usimamizi wa TEHAMA

2015-11-09

Wakala imepokea na kushughulikia maombi 400 kutoka taasisi 107 za umma na kutoa ushauri wa kitaalam na kiufundi katika maeneo ya utengenezaji na uboreshaji wa mtandao wa ndani wa taasisi (Local Area Network), utengenezaji wa mipango mkakati ya kujikinga na majanga (Disaster Recovery Plans), utengenezaji wa mipango mkakati wa TEHAMA (ICT Strategic Plans) pamoja na uwezeshaji na upatikanaji wa Tovuti katika Mtandao wa Intaneti (Search Engine Optimization

Mfumo wa Huduma kwa Wateja

Katika kuboresha huduma zake Wakala imekamilisha mfumo wa huduma kwa wateja ili kuweza kutoa msaada wa kiufundi kwa wataalam wa TEHAMA kutoka taasisi za umma. Huduma hizi hupatikana saa 24 siku saba za wiki (24/7) kwa mwaka. 

Mfumo huu unamwezesha mteja kuwasilisha maombi au matatizo ya kiufundi kupitia http://helpdesk.ega.go.tz, barua pepe egov.helpdesk@ega.go.tz na simu namba +255 764 292 299.

Mafunzo ya TEHAMA

Wakala imetoa mafunzo mbalimbali kwa watumishi wa taasisi za umma yakiwemo usimamizi wa Mtandao wa Mawasiliano Serikalini (Govnet) na mafunzo ya ‘Cyberoam’ kwa taasisi 83 za umma ili kusaidia katika masuala ya utawala, uendeshaji na matengenezo ya mtandao huo. Mafunzo mengine ni ya Uendeshaji wa Vituo vya Data na Usimamizi wa Mfumo wa Baruapepe Serikalini (GMS) kwa watumishi 162 kutoka taasisi 91 za umma yaliyolenga kuongeza uwezo wa kutoa huduma bora katika matumizi ya mfumo huo. Aidha, Wakala imetoa mafunzo ya usimamizi wa taarifa za tovuti na maudhui yake kwa taasisi 50.

 Mafunzo kwa Vitendo

Wakala imetoa fursa kwa watumishi saba (7) kutoka kwenye taasisi mbalimbali za Serikali kufanya kazi ndani ya Wakala kwa lengo la kujifunza kwa vitendo kuhusu utekelezaji wa Serikali Mtandao.

Mawasiliano na Wadau

Wakala imeandaa Mpango Mkakati wa Mawasiliano (Communication Strategy) utakaoisadia kuwasiliana na wadau wake. Aidha Wakala imetumia fursa mbalimbali kuelimisha wadau kuhusu utekelezaji wa Serikali Mtandao  kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii