Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Sisi ni nani?

Sisi ni nani?

Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) ni Taasisi ya Serikali iliyoundwa kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30, Sura ya 245 ya mwaka 1997. Wakala imeundwa kama sehemu ya utekelezaji wa uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa mwaka 2004 kuhusu uanzishwaji wa Serikali Mtandao; na Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu Na. 51 wa tarehe 17 Desemba mwaka 2010 ambao umeipa jukumu na mamlaka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kutayarisha Sera ya Serikali Mtandao na kuhakikisha utekelezaji wake kwa kuanzisha Wakala ya Serikali yenye jukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania. Wakala ilianza kazi ya kutekeleza majukumu yake tarehe 01/04/2012 na kuzinduliwa rasmi mwezi Julai 2012.

Dira

Kuwa Taasisi inayoongoza kiubunifu, katika kuwezesha matumizi ya TEHAMA kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma.

Dhamira

Kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya uratibu, usimamiaji na uendelezaji wa matumizi ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa Umma.

Kaulimbiu

Uwezeshaji Wananchi kwa kutumia TEHAMA

Misingi Mikuu
Uadilifu

Wakala inafuata viwango vya uendeshaji vya hali ya juu katika kila inachofanya na inatimiza ahadi zote kwa maslahi ya Taifa.

 

Ubunifu

Tunaamini kuwa ubunifu na fikra sahihi zinawezesha Wakala kuwa taasisi kinara na mwezeshaji katika utoaji wa huduma za Serikali Mtandao kwa wadau wa Taasisi za Serikali zinazojitegemea.

 

Kuthamini Wateja

Tunaamini katika uwezo wa kila mfanyakazi kuendelea kujifunza kuhusu wateja na kuwahudumia ipasavyo kulingana na mahitaji wanayotarajia kutoka Wakala ya Serikali Mtandao. 

 

Ushirikiano

Wakala inaamini kuwa kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano na wadau muhimu kutaiwezesha kutoa huduma bora zaidi.

 

Mwenendo Bora

Tunaamini kwa kushirikiana na wadau wengine, tunaweza kujenga mfumo bora wa utendaji unaoweza kuigwa na taasisi nyingine za umma.