Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Vitengo

Vitengo

Habari, Elimu na Mawasiliano

Kinasimamia shughuli zinazohusiana na vyombo vya habari , Uhamasishaji, huduma za masoko, usimamizi wa maudhui ya tovuti na matukio, uhusiano na kutoa msaada unaohitajika kwa programu za idara, vitengo na sehemu kwa masuala yanayohusika ya eGA.Sheria

Kinatoa  msaada wa kisheria, ushauri, utaalamu na huduma kwa idara, vitengo, sehemu za wakala na taasisi nyingine.

Sheria

Kinatoa  msaada wa kisheria, ushauri, utaalamu na huduma kwa idara, vitengo, sehemu za wakala na taasisi nyingine.

Ununuzi

Kinatoa utaalamu, ushauri na huduma kuhusu ununuzi, uhifadhi na ugavi wa bidhaa na huduma kwa Wakala.

Usimamizi wa Fedha

Inatoa utaalam na huduma kuhusu masuala ya usimamizi na utunzaji wa fedha kwa Wakala.

Ukaguzi wa Ndani

Kinatoa  huduma za ushauri kwa Ofisa Masuuli kuhusu usimamizi mzuri wa rasilimali.

 

Mipango na Maendeleo

Kinaandaa mipango mikakati na kusimamia utendaji kazi wa Wakala, utafiti wa kitaifa unaosimamia Serikali Mtandao.

Utafiti na Mafunzo

Kinaratibu na kuendesha shughuli za utafiti zinahusiana na ubunifu kuhusu Utekelezaji wa Serikali Mtandao kwa utoaji bora wa huduma kwa umma na kutoa elimu na stadi zinazohitajika kwa viongozi wa taasisi za umma kwa ajili ya upangaji, utekelezaji, usimamizi mzuri na uendelevu wa Jitihada za Serikali Mtandao.