Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Mfumo wa Kujisajili kwa ajili ya Mkutano

Mfumo wa Kujisajili kwa ajili ya Mkutano

Jinsi ya Kujisajili kwa Ajili ya Mkutano

Kila mshiriki anatakiwa kujisajili kupitia kwenye mfumo wa Mkutano wa Serikali Mtandao 2019 au kupitia tovuti ya Wakala ya Serikali Mtandao sehemu ya Kikao Kazi 2019. Baada ya kujisajili utapata Kumbukumbu Namba (Control Number) itakayokuwezesha kufanya malipo ya ada ya ushiriki kupitia Mfumo wa Malipo ya Serikali Kielektroni (GePG) kwa Benki au kwa Mitandao ya Simu.

Utaratibu wa Malipo

•Lipa kwa T-pesa, M-pesa, Airtel-Money, Tigopesa, Z-pesa na Halopesa.

•Benki ya NMB ikiwa ni pamoja na kuwezesha kufanya uhamisho wa fedha kutoka benki nyingine yoyote.

 

Unaweza kulipa kwa kuhamisha fedha moja kwa moja kutoka katika Benki yoyote kwenda kwenye Akaunti yetu iliyoko Benki ya NMB kwa njia ya TISS / SWIFT jaza

1.         Namba ya Akaunti  kwenye Field 59

2.         Kumbukumbu ya Malipo (Payment control number) kwenye  Field 70

Lipa Kupitia Mitandao ya Simu:

•           TTCL  T-pesa

i.           Piga *150*71#

ii.          Chagua 5 – Lipa Bill.

iii.         Chagua 3 – Malipo ya Serikali.

iv.         Weka namba ya kumbukumbu (Control number).

v.          Weka namba yako ya siri.

vi.         Thibitisha malipo.

 

•           Vodacom M-pesa

i.           Piga *150*00#

ii.          Chagua 4 – Lipa kwa M-pesa.

iii.         Chagua 5 – Malipo ya Serikali.

iv.         Chagua 1 – Namba ya malipo.

v.          Weka namba ya malipo (Control number).

vi.         Weka namba yako ya siri.

vii.        Thibitisha malipo.

 

•           Tigo-pesa

i.           Piga *150*01#

ii.          Chagua 4 – Lipia Bili.

iii.         Chagua 5 – Malipo ya Serikali

iv.         Ingiza namba ya malipo (Control number).

v.          Ingiza kiasi.

vi.         Ingiza namba ya siri kuhakiki.

 

•           Airtel Money

i.           Piga *150*60#

ii.          Chagua 5 – Lipia Bili.

iii.         Chagua 5 – Malipo ya Serikali.

iv.         Chagua 1 - Weka namba ya Kambukumbu.

v.          Ingiza Kumbukumbu ya malipo (Control number).

vi.         Kiasi.

vii.        Ingiza namba ya siri kuhakiki.

 

•           Halopesa

i.           Piga *150*00#

ii.          Chagua 4 – Lipa kwa Halopesa.

iii.         Chagua 7 – Huduma za Serikali.

iv.         Ingiza kumbukumbu namba (Control number).

v.          Weka namba yako ya siri.

vi.         Thibitisha malipo