Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Miongozo na Viwango

Kanuni za Viwango na Miongozo
Kanuni Sababu Hatua za Kufuata

1. Serikali inalenga wananchi wake.

Serikali ipo kuhudumia umma wa Watanzania wanaotaka kupata huduma na taarifa kwa urahisi, haraka na zilizo  nafuu.  

 • Taasisi za umma zitabuni na kutumia michakato ya shughuli na huduma zao kunufaisha wananchi, hata kama huduma hizo zitavuka mipaka ya shughuli zake.
 • Serikali hutoa huduma iliyo sawa, ikipunguza urudufu, utata usio wa lazima na njia zisizotofautiana. 
 • Wananchi wanaweza kupata huduma za Serikali kwa kutumia njia mbalimbali. 

 

2. Serikali ni taasisi moja iliyoungana.

Shughuli moja yenye malengo mkakati shirikishi, utawala wa pamoja, michakato ya usimamizi iliyofungamanishwa na sera thabiti huboresha utekelezaji mikakati na uratibu wa utoaji huduma za serikali kwa wananchi. 

 • Serikali inatenga rasilimali zake ili kutimiza malengo iliyojiwekea. 
 • Serikali inatumia taarifa kwa ukamilifu kwenye shughuli zote ili kusaidia huduma na michakato.
 • Mipango iliyobuniwa hufungamanisha huduma kwa ajili ya kuleta ufanisi na kutoa uhuru wa utendaji wa shughuli kwa ajili ya kuleta mafanikio. 
 • Mipango iliyobuniwa hubainisha na kuruhusu mikabala ya kipekee kudumisha malengo muhimu ya sera. 

 

3. Mfumo wa Serikali unatokana na dhamira mahususi. 

Muundo unaozingatia shughuli hufanikiwa zaidi katika kutumiza malengo ya kimkakati kukidhi mahitaji ya mabadiliko ya dhamira na kuhudumia matarajio ya wananchi. 

 • Muundo wa shughuli uliothibitishwa ni sharti muhimu la uwekezaji, kwa hiyo Wakuu wa Teknolojia ya Habari na watayarishaji mipango ni lazima washauriane na viongozi wa program ili waseme namna itakavyokuwa na kufanya kazi. Muundo huo unategemea zaidi mahitaji ya dhamira ya program na teknolojia wezeshi
 • Taasisi za umma zitatumia kwanza  kikamilifu michakato ya shughuli na halafu  viwango vya utendaji kubainisha mahitaji ya uendeshaji.  
 • Mifumo na michakato itatumia muundo ambao utashughulikia kwa haraka matukio, ikiwemo mbinu za kufikisha taarifa kwa watu wengi wakati mmoja. 
 • Taasisi za umma zitatumia miundo ya taasisi zao kuongoza utayarishaji wa mipango ya maendeleo, bajeti na uamuzi wa uwekezaji.
 • Taasisi za umma zitasimamia mabadiliko ya shughuli za Serikali kwa kuzingatia  usalama wa kutosha kuwezesha huduma kuendelea. 
 • Teknolojia ya habari serikalini  lazima iweze kubadilika kulingana na  mahitaji ya shughuli

 

4. Usalama, faragha na kulinda taarifa ni mahitaji ya msingi ya Serikali 

Serikali lazina ilinde taarifa zake za  siri ili kuongeza Imani ya wananchi na kuboresha usalama wa rasilimali zake. 

 • Muktadha wa shughuli unaainisha mahitaji ya usalama na faragha, unaojumuishwa katika muundo wakati wa kipindi chote cha shughuli.  
 • Miundo ni lazima ionyeshe sera ili kupunguza matumizi mabaya ya data na ukiukaji wa usalama.
 • Serikali ni lazima itumie viwango vya usalama na faragha wakti wote na kufuatilia utimizaji.
 • Kanuni za usalama wa taarifa ni lazima ziwekwe wazi ili kuwianisha na kudhibiti gharama na  vihatarishi

 

5.Taarifa ni rasilimali ya Taifa. 

Wananchi arifu ni muhimu kwa demokrasia.  Aidha taarifa sahihi ni muhimu katika utoaji uamuzi wenye tija, utendaji bora na utoaji sahihi wa taarifa. 

 

 • Serikali itaboresha mazingira ya upashanaji taarifa ili kusambaza vizuri zaidi taarifa kwa umma. 
 • Hii inahitaji kubainisha vyanzo vyenye mamlaka ya taarifa za ubora wa hali ya juu na taasisi za umma kuruhusu upataji wa data na taarifa mahususi.              
 • Vyanzo vya data vyenye mamlaka ni lazima viundwe upya na kuorodheshwa kwa ajili ya usambazaji, upataji na usimamizi rahisi. 
 • Kutimiza kanuni hii kunahitajika mkakati wa serikali kuhamasisha uenezaji data wa gharama nafuu ndani na kwenye taasisi zote.   

 

6.Muundo unarahisisha utendaji wa Serikali.

Mifumo na michakato tata yenye moduli zilizounganishwa ni migumu kusimamia,rahisi kushindwa,haibadiliki kuendana na mahitaji ya dhamira ya wakala na ni ghali kuendesha.  Mifumo ya moduli nyingi na michakato isiyounganishwa hunufaishwa na huduma shirikishi  na mifumo inayotumika tena  ndani ya serikali na kupatikana kibiashara.  

 

 • Hii inahitaji mifumo tumizi isiyounganishwa inayotumiwa kama huduma na uendelezaji wa program zinazopatana. 
 • Taasisi za umma ni lazima zishirikiane mienendo bora na mifumo ya shughuli na ya kiufundi inayotumika tena. 
 • Kuunda na kujumuisha mifumo inayotumika tena  ni lazima iwe ni njia ya kawaida ya uendelezaji.