Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Nifanyeje...

Nifanyeje...

Kusajili au Kuhamisha Anuani ya ".go.tz"

Wakala ya Serikali Mtandao ni msajili pekee wa majina ya mitandao yote ya .go.tz na .mil.tz, hivyo  ina mamlaka ya kisheria ya kusajili majina yote ya mitandao kwa Taasisi za Serikali. Hii ni katika kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA (2003). K wa taarifa zaidi tafadhali pakua Viwango vya Majina ya Anwani za Tovuti za Serikali

 Masharti:

1. Taasisi ya Umma

2. Fomu ya Usajili wa anwani za tovuti (Pakua hapa) 

3. Fomu ya Kuhamisha Anwani za Tovuti Pakua hapa

4. Ada ya Usajili/ Uhamisho wa anwani za tovuti kwa mwaka ni Tsh. 25,000/=

Taratibu

1. Jaza fomu ya usajili au Uhamisho wa anwani ya tovuti 

2. Lipa ada ya usajili/ uhamisho wa anwani za tovuti kupitia Akaunti ya Mapato ya Wakala (e-Government Agency Revenue A/C) Na.          20110002340, NMB Bank baada ya kupata namba ya kumbukumbu ya malipo.

3. Ambatisha fomu ya usajili/ uhamisho wa anwani ya tovuti pamoja na fomu ya kulipia benki

4. Wasilisha fomu hiyo kupitia barua pepe (egov.helpdesk@ega.go.tz) /(info@ega.go.tz) au S.L.P 4273 DSM.