Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Nifanyeje...

Nifanyeje...

Kutengeneza Tovuti

Maendeleo ya haraka ya teknolojia ya habari na  mawasiliano (TEHAMA) katika miaka ya hivi karibuni yamewezesha upatikanaji na usambazaji wa taarifa katika jamii. Taasisi na watu wengi zaidi wameamua kutumia  tovuti kama njia inayofaa zaidi  na ya gharama nafuu ya usambazaji na upatikanaji wa taarifa duniani kote. Kwa hiyo taasisi za umma zinashauriwa kutengeneza na kuendesha tovuti kurahisisha utoaji wa taarifa na huduma kwa wananchi. Hata hivyo tovuti hizo zinatakiwa kutengenezwa kwa kufuata miongozo, viwango na mwenendo bora.

  Masharti

1. Anuani ya jina la tovuti lililosajiliwa

2. Andika barua ya maombi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao

3. Wasilisha mahitaji yako ya tovuti ya mwisho, kwa mfano mchoro unaoonesha mpangilio wa taarifa

5. Hudhuria mafunzo ya siku tano kuhusu usimamizi wa taarifa zinazowekwa kwenye tovuti.

7. Baada ya malipo hayo, utakabidhiwa tovuti yako rasmi.

Zingatia:                          

1. Iwapo anuani ya tovuti yako inahifadhiwa na kuhudumiwa mahali pengine, ni lazima uiwasilishe kwa Wakala.

2. eGA itaendelea kutoa msaada wa kiufundi kwa tatizo lolote wasiliana nasi kupitia barua pepe: egov.helpdesk@ega.go.tz au piga namba +255 764 292 299