Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Nifanyeje...

Nifanyeje...

Kutengeneza Mfumo

eGA inatengeneza mifumo mbalimbali ya habari na mifumo tumizi kukidhi mahitaji mbalimbali ya  shughuli za taasisi.  Baada ya maombi kupokewa tunashirikiana kwa karibu na Mteja kuhakikisha kuwa huduma tutakayompa inatimiza matakwa yake. 

Masharti:

1. Malengo mahususi ya mfumo 

2. Ainisha iwapo Mfumo utakuwa na Tovuti au la

Taratibu:  

1. Andika barua ya maombi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao

2. Hudhuria mkutano wa kukusanya mahitaji ya mfumo kwenye ofisi za eGA

3. Baada ya mfumo tumizi kukamilika, utawasilishwa kwako

4. Hudhuria mafunzo ya usimamizi wa mfumo huo

5. Lipa ada ya utengenezaji Mfumo Tumizi inayostahili kupitia Akaunti ya Mapato ya Wakala (e- Government Agency Revenue A/C) Na.     20110002340, NMB Bank.

6. Baada ya malipo hayo, Mfumo Tumizi utakabidhiwa kwako rasmi.