Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Nifanyeje...

Nifanyeje...

Kuunganishwa na Mfumo wa Barua Pepe Serikalini

Mfumo wa Barua pepe wa Serikali (GMS) ni mfumo unaowezesha mawasiliano na kubadilishana taarifa kati ya taasisi na taasisi Serikalini kwa usalama.

Masharti:

1.  Anuani ya tovuti iliyosajiliwa inayofuata mwongozo katika viwango vya Serikali kwa matumizi sahihi ya TEHAMA, kwa mfano, .go.tz

2. Anuani ya tovuti kwa ajili ya akaunti ya barua pepe inayohifadhiwa na eGA.

3. Uwe na idadi mahususi ya watumiaji wanaotarajiwa kutumia huduma hiyo.

 Taratibu:

1.   Barua ya maombi

2.   Ainisha idadi ya watumiaji wanaotarajiwa kutumia mfumo huo katika barua yako

3.  Teua wasimamizi wawili wa mifumo watakaohudhuria mafunzo ya Usimamizi wa Mfumo na Uanzishwaji wa akaunti ya GMS katika taasisi yako.

4.   Iwapo anuani ya akaunti yako inahifadhiwa na kuhudumiwa mahali pengine, ni lazima uwasilishe ufunguo wa uhawilishaji.

5.  Lipa ada ya mwaka inayostahili kulingana na idadi ya watumiaji kupitia Akaunti ya Wakala (e-Government Agency A/C) Na. 20110002340, NMB Bank.