Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Nifanyeje...

Nifanyeje...

Ugawaji wa Bandwidth

“Bandwidth” ya kimataifa ni kiwango cha juu cha utumaji data kutoka nchi moja kwenda nyingine. Serikali ya Tanzania kupitia Mradi wa Muundombinu wa Mawasiliano ya Tanzania na Mradi wa Serikali Mtandao (RCIP Tanzania) imenunua Hati ya Matumizi Isiyotanguka (IRU) ya 1.55 Gbps ya “Bandwidth” ya Kimataifa itakayotumiwa na Taasisi za Umma kwa kipindi cha miaka 10.

Masharti:

1. Fomu ya kubainisha mahitaji ya mteja iliyojazwa

2.   Ni lazima uwe umeunganishwa na mkongo wa mawasiliano kupitia TTCL

3.  Ni lazima uwe Taasisi ya Umma.

Taratibu:

1. Andika barua ya maombi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao.

2. Jaza fomu kuainisha kiasi cha "Bandwidth"kinachoombwa

4. Maombi ya “Bandwidth” yatatathminiwa na utapewa majibu ya mahitaji yako kulingana na matumizi 

5. "IP address” na “Bandwidth” iliyoombwa itagawiwa kwenye taasisi yako.

6. TTCL itaiweka na kuijaribuiliyogawiwa katika taasisi yako