Mwongozo huu ni maelekezo ya kiufundi kwa Taasisi za Umma na watumishi wa Serikali kufuata maagizo kuhusu matumizi ya TEHAMA na vifa vinavyohusiana.
Mwongozo huu unaeleza masharti, viwango na miongozo kwa ajili ya utekelezaji wenye mfanikio na matumizi ya Mfumo Jumuishi wa Kielektroni wa Usimamizi wa Vituo vya Kutolea Huduma za Afya vya umma na vya binafsi nchini Tanzania. Pia unaeleza muundo wa uongozi na utawala katika Kamati ya Taifa ya Uendeshaji wa afya mtandao (NeHSC) utakao saidia kuhakikisha utekelezai wa jitihada za afya mtandao kwa wakati.
MWONGOZO WA MATUMIZI BORA, SAHIHI NA SALAMA WA VIFAA, DATA NA MIFUMO YA TEHAMA SERIKALINI.