Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Ushauri na Msaada

Ushauri na Msaada

Kutokana na ongezeko la matumizi sahihi ya TEHAMA kwa umma yaliyochagizwa na maendeleo ya teknolojia na hivyo kuongezeka kwa ushirikiano miongoni mwa taasisi za umma (G2G), Serikali na Wananchi (G2C), Serikali na Watumishi (G2E) na Serikali na Biashara (G2B), Serikali ililazimika kutegemea wakandarasi kwa huduma za ushauri wa kitaalam na msaada wa kiufundi. Hali hiyo iliilazimu Serikali kutumia gharama kubwa na kukosa udhibiti wa mifumo.

Katika kipindi cha taarifa hii, Wakala imetoa ushauri kwa taasisi za umma 299 na msaada wa kiufundi 2,947 katika maeneo ya uhakiki wa Mifumo ya TEHAMA, Tathmini ya Usalama, Utayarishaji wa Mpango wa Kukabili Majanga, Utayarishaji wa Sera ya TEHAMA, Utayarishaji wa Mkakati wa TEHAMA, Usanifu na Tathmini ya Miradi ya TEHAMA.

Msaada wa Kiufundi

Katika kuhakikisha huduma zake zinashamiri, Wakala imetengeneza na kuendesha Mfumo wa Huduma kwa Mteja ili kuwezesha na kuboresha utoaji wa msaada wa kiufundi kwa taasisi za umma. Mfumo huu unapatikana wakati wote yaani 24/7/365.