Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Mkutano wa Pili wa Serikali Mtandao 2019

Mkutano wa Pili wa Serikali Mtandao 2019

Mkutano wa Pili wa Serikali Mtandao utafanyika kwa siku 4 mfululizo kuanzia tarehe 30 Januari hadi tarehe 2 Februari, 2019 katika Ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano - Chuo Kikuu cha Dodoma.

Mkutano utakuwa wa Awamu Tatu: Awamu ya kwanza itakuwa ya muda wa siku mbili, tarehe 30 na 31 Januari, 2019 na kuwashirikisha Maofisa TEHAMA, Maofisa Ununuzi, Maofisa Mawasiliano Serikalini, Maofisa Utumishi, Maofisa Utawala na Watumiaji Mifumo. Awamu ya Pili itakuwa tarehe 1 Februari, 2019 na kuwashirikisha Maofisa Masuuli wa Serikali Kuu na Mamlaka ya Serikali za Mitaa na Awamu ya Tatu ni tarehe 2 Februari, 2019 na itahusisha washiriki wote waliojisajili kwa ajili ya Siku ya Utafiti na Ubunifu ya Serikali Mtandao.