Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Ushauri, Uelekezi na Msaada wa Kiufundi

Ushauri, Uelekezi na Msaada wa Kiufundi

Wakala inatoa huduma za ushauri wa kitaalamu na msaada wa kiufundi kuhakikisha kuwa TEHAMA inasimamiwa ipasavyo, inawekezwa, kuendeshwa na kudumishwa ipasavyo kutimiza malengo ya kimkakati ya taasisi.

Huduma zinatolewa katika maeneo ya Uhakiki wa Mifumo ya TEHAMA, Tathmini ya Usalama, Utayarishaji wa Mpango wa Kukabili Majanga, Utayarishaji wa Sera ya TEHAMA, Utayarishaji wa Mkakati wa TEHAMA, Usanifu na Tathmini ya Miradi ya TEHAMA.

 Manufaa

a) Huboresha uwezo, ufanisi na gharama nafuu

b) Huwezesha uzingatiaji na ufuataji wa viwangovya Serikali Mtandao

c) Husaidia uwianishji wa jitihada za Serikali Mtandao

 Masharti

a) Lazima iwe taasisi ya Serikali

b) Lazima iwe na upeo mahususi na matokeo ya kazi unayotaka kuifanya (T.O.R)

c) Onesha muda mahususi wa kazi

 Taratibu

a) Wasilisha barua ya maombi kwa Mtendaji Mkuu eGA

b) Utaalikwa kwa ajili ya uelewa wa awali na mahitaji

c) Utatia saini mkataba wa maandishi

d) Lipa ada iliyokubalika kwenye Akaunti ya Wakala No 20110002340 katika Benki ya NMB

e) Utekelezaji wa kazi

f) Uwasilishaji wa taarifa ya mshauri kwa mteja.