Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Hudma kwa Wateja

Hudma kwa Wateja

Ni mahali pa mawasilano (SPOC) ya kupokea na kutoa msaada wa kiufundi kwa taasisi za umma.Hujumuisha misaada yote ya kiufundi ikiwemo utoaji taarifa na ufuatiliaji wa maombi au matukio yaliyotolewa taarifa.Ni mawasiliano baina ya Serikali kwa Serikali (G2G) ikisaidiwa na njia nyingine za mawasiliano.

Mfumo huu unawezesha wateja kuingia au kupiga simu na kutoa taarifa ya tukio kwa kutengeneza tiketi na kuipa namba ya kumbukumbu. Wateja wanaweza kutuma au kuwasilisha mrejesho wao kuhusu huduma iliyotolewa 24/7. Mfumo unatoa fursa ya kuchagua aina ya huduma na unaeleza hali ya ombi au tukio na kuhakikisha msaada na mrejesho unaohitajika.

Manufaa

a) Huwezesha taasisi za umma kuwasilisha masuala ya kiufundi ya TEHAMA kwa urahisi na haraka na kutanzuliwa kwa wakati mwafaka na ufanisi

b) Mfumo unashughulikia mtiririko wa ufumbuzi wa masuala ya kiufundi, kutunza taarifa na kumuarifu mhusika. 

c) Inatunza kumbukumbu ya masuala yote yaliyowasilishwa, inarahisisha ufuatiliaji na kutoa taarifa ya kilichofanyika 

d) Hutoa nafasi kwa watumiaji kutayarisha tiketi, kupitia utekelezaji wa yaliyofunguliwa na kufunga tiketi mara baada ya kutanzuliwa

Masharti

a) Lazima iwe taasisi ya umma

b) Lazima uwe na anwani ya baruapepe iliyofunguliwa mf. ictsupport@fqdn...

c) Lazima uwe na maelezo kamili ya tukio linatotolewa taarifa.

d) Ambatisha jalada la tukio lililotolewa taarifa kwa ufafanuzi wakati wa kutanzua.

Taratibu

 a) Andika barua kwa Mtendaji Mkuu eGA

 b) Ambatisha jalada la tukio na uliwasilishe

c) Mnakili Msimamizi/Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA au Ofisa Masuuli.