Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Rasilimali Shirikishi ya TEHAMA

Rasilimali Shirikishi ya TEHAMA

Wakala imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya kusanifu ujenzi wa kituo kidogo cha kuhifadhi na kuendesha  mifumo mbalimbali ya Serikali Mtandao. Kuwepo kwa kituo hiki kutasaidia upatikanaji wa uhakika wa mifumo ya Serikali Mtandao kwa watumiaji na kuwezesha mifumo hiyo kuhifadhiwa sehemu moja badala ya illivyo sasa ambapo uhifadhi wa mifumo umetawanyika katika sehemu mbalimbali.