
Usajili wa Anwani za Tovuti za Serikali
Usajili wa Anwani za Tovuti za Serikali
Wakala ya Serikali Mtandao ni msajili pekee wa majina ya mitandao yote ya .go.tz na .mil.tz, hivyo ina mamlaka ya kisheria ya kusajili majina yote ya mitandao kwa Taasisi za Serikali. Hii ni katika kutekeleza Sera ya Taifa ya TEHAMA (2003).
Masharti:
- Fomu ya Usajili wa anwani za tovuti (Pakua hapa)
- Ada ya Usajili wa anwani za tovuti kwa mwaka ni Tsh. 25,000/=
Taratibu
- Jaza fomu ya usajili wa anwani ya tovuti
- Lipa ada ya usajili wa anwani za tovuti kupitia Akaunti ya Mapato ya Wakala (e- Government Agency Revenue A/C) Na. 20110002340, NMB Bank.
- Ambatisha fomu ya usajili wa anwani ya tovuti pamoja na fomu ya kulipia benki
Wasilisha fomu hiyo kupitia barua pepe (info@ega.go.tz) au S.L.P 4273 DSM.
Kwa maelezo zaidi bofya hapa