Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Kuhifadhi Mifumo ya TEHAMA

Kuhifadhi Mifumo ya TEHAMA

Serikali inaboresha mazingira ya kuhudumia na kuhifadhi mifumo ya habari ili kuwezesha ushirikiano wa nyenzo za TEHAMA baina ya taasisi za umma. Kuna aina mbili za huduma hizo: aina ya kwanza ambayo pia hujulikana kama ‘utangamano’ hutoa fursa ya kuhudumia programu tumizi na mitambo inayohitajika kuendesha programu hizo. Aina ya pili ni  taasisi kuamua kuhudumia programu tumizi tu wakati mitambo inatolewa na eGA.

Masharti:
 • Mfumo wa TEHAMA
 • Mfumo wa TEHAMA uliohakikiwa na Kurugenzi ya Udhibiti wa Huduma za TEHAMA
 • Uwe na “Bandwidth” mahususi inayohitajika
 • Ainisha Teknolojia iliyotumika kwa mfano, Mfumo wa Uendeshaji, Lugha ya kuprogramia, Mfumo wa Menejimenti ya kanzidata
 • Eleza nafasi, ukubwa na Idadi ya watumiaji wa mfumo wako
 • Lazima uwe na msimamizi wa mfumo.
Taratibu:
 • Andika barua ya maombi kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao
 • Eleza kama seva tumizi itahudumiwa na eGA au iwekwe kwenye nafasi ya seva ya eGA
 • Hudhuria mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ya kusimamia mfumo wako 
 • Tia saini mkataba wa maandishi kuhusu huduma ya kuhifadhi mifumo
 • Lipa ada ya huduma inayostahili kupitia Akaunti ya Mapato ya Wakala (e-Government Agency A/C)  Na. 20110002340, NMB Bank.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa