Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Usajili wa Namba za SMS/USSD

Usajili wa Namba za SMS/USSD

Serikali kwa kutumia Wakala ya Serikali Mtandao inaboresha upataji wa huduma za mtandao kwa umma kwa kurasimisha na kuwezesha matumizi ya simu za mkononi na huduma za mtandao Serikalini. Kwa hiyo Taasisi za Umma zinazohitaji kutumia Huduma za Simu za Mkononi kwa kuwahudumia wananchi kwa kutumia vitumi vya mkononi zinahitaji Msimbo mfupi kwa Mfumo wa Ujumbe Mfupi (sms) na Huduma za Data za ziada (USSD).  Aidha, eGA ina jukumu la kuwezesha ugawaji wa Misimbo mifupi kutoka kwenye kundi la akiba ya Misimbo la Serikali. 

Masharti:
  • Fomu 1 iliyojazwa kwa ukamilifu miradi ya sasa na iliyopangwa;
  • Andiko la mradi / Maelekezo ya Dhana
Taratibu:
  • Wasilisha barua ya Maombi iliyotiwa saini;
  • Ambatisha andiko la Mradi/ Maelezo ya Dhana likionyesha uchanganuzi wa hali ilivyo, vipengele muhimu vya mradi kama vile:
  • Madhumuni ya Mradi
  • Taja na fafanua vipengele muhimu vya mradi vinavyojumuisha:
  • Lengo la mradi (lilingane na Malengo ya Mpango Mkakati)
  • Matokeo ya mradi yanayochanganua vipengele muhimu vya gharama kama vile chanzo na thamani ya gharama za utekelezaji, chanzo na gharama za uendeshaji na mpango unaoeleweka wa namna wadau (hasa wadau wa msingi) watakavyoshirikishwa kwenye mradi
  • Mpango wa utekelezaji na uendeshaji wa mradi na uendelevu wake 
Zingatia:

Taasisi ya Umma haina budi kugawiwa Msimbo mfupi na eGA, halafu kuendelea na kuomba CHETI CHA UMILIKI WA NAMBA kutoka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kabla ya kutoa huduma iliyokusudiwa.

Kwa taarifa zaidi bofya hapa