Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Ujumbe wa Mtendaji Mkuu

Ninayo furaha kukukaribisha katika tovuti hii kwa niaba ya watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao Tanzania,  ambapo  tunaamini utapata taarifa za kuaminika na kwa ukamilifu kuhusu wigo, upeo wa mamlaka, dira, dhamira, misingi mikuu, malengo, mikakati, shughuli, ahadi na maadili  ya Wakala.

Taarifa nyingine utakazoona na kusoma ni pamoja na tovuti na mifumo mbalimbali iliyotengenezwa na Wakala, Miongozo na Viwango vya Serikali Mtandao, Ratiba ya Mafunzo na Semina zilizopita na zijazo, Sera, Mpango Mkakati wa mwaka 2012/13 hadi 2016/17 na wa mwaka 2016/17 hadi 2020/21), Vipeperushi, Kitabu cha Huduma za Wakala, Fomu za Ahadi ya Uadilifu na Mkataba wa Huduma kwa Wateja.

Uzinduzi wa tovuti yetu uliofanyika miaka takribani mitano iliyopita ni tukio la kihistoria katika kufikia Dira na matarajio yetu ya kutambuliwa kama taasisi inayoongoza kwa ubunifu, inayowezesha matumizi ya TEHAMA kwa kuboresha utoaji wa huduma kwa umma unaofanywa na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Mamlaka, Wakala na Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini Tanzania.

Wakala inajitahidi kudumisha na kutumia mafanikio makubwa ya Serikali Mtandao yaliyopatikana kwenye Kurugenzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliyokuwa na wajibu wa kusimamia na kuratibu jitihada za Serikali Mtandao kabla ya kuanzishwa kwa Wakala hii.

Lengo letu ni kukabiliana na hali halisi kama ilivyo, kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano na Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka, Mamlaka ya Serikali za Mitaa na wadau wengine katika kutafuta ufumbuzi na njia za kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa umma kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano.

Tovuti hii imetengenezwa kwa ubunifu wa hali ya juu na ni rahisi kutumia na kupata taarifa kwa anayeitembelea. Ni matumaini yangu kuwa, kila atakayetembelea atapata jambo la kujifunza na atarudi tena na tena ili kuendelea kudumisha mawasiliano.

Ukitembelea tovuti hii utabaini mikakati mbalimbali inayotafsiri dhamira yetu katika uhalisia na juhudi zinazochukuliwa na Wakala katika kutimiza malengo kama yanavyotafsiriwa kwenye Mpango Mkakati wa Miaka mitano (2016/17 hadi 2020/21).

Ninaamini kuwa umenufaika kwa kutemebelea tovuti hii, nakuhakishia kuwa tutaendelea kuboresha tovuti hii kadri muda unavyokwenda ili kukidhi matarajio yako kwa ubora wa hali ya juu.

Mtendaji Mkuu

Wakala ya Serikali Mtandao