Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Sisi ni nani?

Sisi ni nani?

Kabla ya kuanzishwa Wakala ya Serikali Mtandao, matumizi ya TEHAMA Serikalini yalikuwa yanaratibiwa na kusimamiwa na Idara ya Usimamizi wa Mifumo (DMIS) iliyopo Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambayo kwa sasa ni Idara ya Huduma za TEHAMA Serikalini (DICTS). Wakala ilianza kufanya kazi Aprili 2012 na kuzinduliwa rasmi Julai 2012.   

Dira

“Kuwa Taasisi inayoongoza kiubunifu, katika kuwezesha matumizi ya TEHAMA kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma kwa Umma.”

Dhamira

”Kujenga mazingira wezeshi kwa ajili ya uratibu, usimamiaji na uendelezaji wa matumizi ya TEHAMA ili kuboresha utoaji wa huduma za Serikali kwa Umma."   

Motto 

“Uadilifu na Ubunifu katika utoaji huduma kwa umma."

Misingi Mikuu

Wakala inaongozwa na misingi mikuu mitano ambayo inaelekeza kuhusu tabia na mwenendo wa watumishi wa Wakala kwa ngazi zote. Misingi hiyo inafafanua utamaduni wa mahali pa kazi, kuhakikisha kuwa watumishi wote na wateja wa Wakala wanauelewa wa pamoja wa jinsi wanavyotakiwa kuhudumiwa na nini kichotarajiwa kutoka kwao. Misingi mikuu hiyo ni pamoja na::-   

Uadilifu:

Wakala inafuata viwango vya uendeshaji vya hali ya juu katika kila inachofanya na inatimiza ahadi zote kwa maslahi ya Taifa.  

Ubunifu;

Tunaamini kuwa ubunifu na fikra sahihi zinawezesha Wakala kuwa taasisi kinara na mwezeshaji katika utoaji wa huduma za Serikali Mtandao kwa wadau wa Taasisi za Umma.

Kuthamini Wateja;

Tunaamini katika uwezo wa kila mfanyakazi kuendelea kujifunza kuhusu wateja na kuwahudumia ipasavyo kulingana na mahitaji wanayotarajia kutoka kwa Wakala ya Serikali Mtandao.

Kufanya kazi kwa pamoja;

Tumedhamiria kutimiza malengo ya pamoja kwa kuzingatia mawasiliano ya wazi na uaminifu, wakati huo huo tukijali na kusaidiana

Ushirikiano

Wakala inaamini kuwa kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano na wadau muhimu kutaiwezesha kutoa huduma bora zaidi.