Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Mfumo wa Baruapepe Serikalini

Mfumo wa Baruapepe Serikalini

Mfumo wa Baruapepe Serikalini ni mfumo salama wa mawasiliano na kubadilishana taarifa Serikalini.

Manufaa:

a) Njia salama ya mawasiliano na inayoaminika Serikalini

b) Mfumo rasmi wa kubadilishana taarifa

c) Unaokoa muda na gharama nafuu

 

Makundi ya Mfumo wa Baruapepe Serikalini:

A) Mfumo Huria wa Baruapepe Serikalini (GMSC)

Wakala ina wajibu wa kuhifadhi na kuendesha mfumo wa baruapepe Serikalini. Taasisi za umma zinachangia kufidia gharama za uendeshaji wa mifumo, kuboresha, kuhifadhi na kuhudumia.

B) Mfumo wa Ndani wa Baruapepe Serikalini (GMSL)

Taasisi zinaweka, simamia na kuendesha mfumo wa baruapepe katika ofisi zao. Mafunzo ya kuweka mpangilio wa seva, uhifadhi na mtandao wa mawasiliano yanatolewa ili kuendesha mfumo kwa ufanisi.

Aina za Akaunti za Mfumo wa Baruapepe Serikalini:

A) Akaunti ya Baruapepe ya Taasisi:

Hutumia kifupisho cah jina la mkuu wa taasisi na kufuatia jina miliki mf. ceo@ega.go.tz or ps@ pmo.go.tz.

 

B) Akaunti ya Baruapepe ya Idara/Kitengo:

Hutumia kifupisho cha jina la Idara/Kitengo ikifuatiwa na jina miliki mf. dims@ega.go.tz. Kwa orodha anwani/makundi mf. group.dims@ega.go.tz

C) Akauti ya Baruapepe ya Mtumishi:

Hutumia mpangilio wa “jinalakwanza.jinalaukoo” ikifuatiwa na jina miliki la taasisi mf. rosa.juma@ega.go.tz. 

Taratibu:

a) Andika barua ya maombi kwa Mtendaji Mkuu wa eGA ukiainisha jina miliki, Namba ya kasma na idadi ya akaunti za baruapepe zinazohitajika

b) Taja majina mawili ya wasimamizi wa mfumo kwa ajili ya mafunzo

c) Wasilisha namba ya kuhamisha iwapo jina miliki limehifadhiwa sehemu nyingine

d) Lipia ada ya mwaka iliyoelezwa kutegemea idadi ya watumiaji kwa kuweka kwenye Akaunti ya Wakala A/C No 20110002340 at NMB Bank.