Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora

Wakala ya Serikali Mtandao.

Kituo cha Utafiti, Ubunifu, Uundaji na Usaidizi wa Mifumo ya Serikali Mtandao (e-GovRIDSC)

Kituo cha Utafiti, Ubunifu, Uundaji na Usaidizi wa Mifumo ya Serikali Mtandao (e-GovRIDSC)

Kituo cha Utafiti, Ubunifu, Uundaji na Usaidizi wa Mifumo ya Serikali Mtandao (e-GovRIDSC) kina lengo la kufanyia utafiti, ubunifu na kuunda mifumo ya TEHAMA ya Serikali Mtandao yenye lengo la kuongeza ufanisi na urahisi kwa huduma pamoja na mifumo ya mbalimbali ya utoaji huduma zitolewazo na Serikali katika sekta zote.  

Dira:

Kuwa mahali panapofaa zaidi kujifunza, kuelimisha, kutafiti, kubuni na kutoa usaidizi wa mifumo ya Serikali Mtandao hivyo kutoa mchango mkubwa kwa Maendeleo ya Kijamii, Kiutamaduni na Kiuchumi nchini Tanzania kupitia uendeshaji shughuli za Serikali kwa ufanisi na utoaji huduma za Umma za hali ya juu kwa kusaidiwa na matumizi ya TEHAMA.

Dhamira:

Kuboresha maisha kwa kutoa huduma bora za Serikali kwa umma zinazoungwa mkono na mifumo ya serikali mtandao iliyo fanyiwa utafiti wa dhati, uchanganuzi, kusambazwa na kupatiwa usaidizi wa kiutaalam

Washiriki Wakuu

Kituo kitahudumia aina tatu (3) za washiriki ambao ni: Watafiti, Wabunifu na Watengeneza Mifumo waliogawanywa katika makundi mawili yafuatayo: 

a) Wanafunzi wa mafunzo kwa vitendo 

  • Wanafunzi wanaosomea mafunzo ya TEHAMA wenye mapendekezo ya mifumo iliyo na tija au watakaopewa kutafiti au kutekeleza mifumo ya serikali mtandao;
  • Wanafunzi wasiosomea mafunzo ya TEHAMA wanaopewa mamlaka ya kutathimini mifumo ya serikali mtandao inayotumiwa na Taasisi za Serikali na kutoa mrejesho kwa ajili ya uboreshaji.

b) Wataalam wa TEHAMA wenye shauku na ujuzi wa ufumbuzi wa mifumo ya Serikali Mtandao na wanaotaka kufanya utafiti au ubunifu au uendelezaji wa mifumo ya huduma za Serikali Mtandao

Kituo kitatoa miongozo kila mara inayotoa mwelekeo wa jinsi ya kushirikishwa katika shughuli zake.