Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Wakala ya Serikali Mtandao.
Wakala ya Serikali Mtandao ni taasisi ya Serikali yenye jukumu na mamlaka ya kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao katika utumishi wa umma.
Huduma zetu zinalenga kuboresha utoaji taarifa na huduma kwa umma kwa njia ya mtandao kwa uwazi, urahisi na kwa gharama nafuu.
eGA inaandaa miundombinu inayohitajika kusaidia jitihada za Serikali mtandao katika sekta mbalimbali zinazolenga kutoa huduma kwa njia ya mtandao kwa wakati, urahisi na kwa gharama nafuu.
Wakala inachapisha taarifa za kiutendaji na inatoa vipeperushi mbalimbali ambavyo vinaonyesha jitihada za utekelezaji wa shughuli za Serikali Mtandao kwa umma.
eGA inanunua huduma au bidhaa zenye ubora, kwa wakati na kwa gharama nafuu ili kukudhi mahitaji yake kwa kuzingatia Sheria ya ununuzi Na.7 ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2013.
Sehemu hii inakupa hotuba, taarifa kwa vyombo vya habari, video na picha za matukio mbalimbali.
eGA inatoa mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo Maofisa Tehama na watumishi wengine wa taasisi za Serikali ili kurahisisha utekelezaji na jitihada za Serikali Mtandao nchini Tanzania.
Mkataba wa Huduma kwa Wateja
Mkataba wa Huduma kwa Wateja 2015/16
Kwa msaada wa kiufundi kuhusu huduma za Wakala ya Serikali Mtandao, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe: egov.helpdesk@ega.go.tz
eGA inashauri taasisi zote za Umma kusajili majina ya anuani ya tovuti zao kwa “.go.tz” ikiwa ni pamoja na zinazotumia ".com au .org"
Tembelea Tovuti Kuu ya Serikali kwa anuani ya www.tanzania.go.tz inayokuwezesha kupata taarifa na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.