emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Kikao Kazi cha 2 cha Serikali Mtandao 2019

2019-01-30 To 2019-02-02 | Venue | UDOM - Dodoma

Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) iliandaa Kikao Kazi cha pili cha Serikali Mtandao kilichofanyika Januari 30 hadi Februari 2, 2019 katika ukumbi wa Chuo cha Sayansi ya Kompyuta, Habari na Mawasiliano uliopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa lengo la kuonesha jitihada mbalimbali za Serikali Mtandao zilizofanyika, zinazoendelea na zilizopangwa kufanyika ndani ya Serikali, changamoto na fursa zilizopo na kuzitatua. Katika kikao hicho wadau wa serikali mtandao walibadilishana uzoefu, kujadili njia mbalimbali na kutatua changamoto na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu serikali mtandao.

Kaulimbiu

Uwianishaji wa Rasilimali za TEHAMA kwa Maendeleo ya Viwanda

Angalia Nyaraka Angalia Programu

Wahusika

Kikao hicho kilihudhuriwa na washiriki 786 kutoka taasisi za umma waliogawanyika katika makundi matatu. Kundi la kwanza lilifanya kikao tarehe 30 - 31 Januari, 2019 ambalo lilihusisha Maofisa TEHAMA na Maofisa wanaotumia mifumo ya TEHAMA. Kundi la pili lilifanya kikao cha tarehe 01 Februari 2019 na lilihusisha Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Kundi la tatu lilihuhusisha washiriki wa makundi yote (Kundi la kwanza na la pili) pamoja na Wabunifu na Watafiti kutoka Vyuo Vikuu na Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Teknolojia. Kundi hili la tatu lilihudhuria Kikao cha siku maalumu ya Utafiti na Ubunifu katika eneo la utekelezaji wa Serikali Mtandao tarehe 2 Februari 2019

Aidha, Washiriki waligawanyika katika makundi na kujadiliana changamoto hizo kwa kina na kuainisha mbinu na fursa ikiwemo kuandaa mpango kazi utakao ongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao. Aidha, Katika Kikao cha kundi la tatu ambacho kilikuwa maalum kwa ajili ya Utafiti na Ubunifu wa Serikali Mtandao, ambapo Vyuo Vikuu, Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Teknolojia na Taasisi za Utafiti nchini vilialikwa kuwasilisha bunifu na tafiti katika serikali mtandao. Jumla ya Tafiti/Bunifu 24 ziliwasilishwa. Tafiti/Bunifu 10 zilichaguliwa kushi.riki maonesho wakati wa kikao kazi hicho.

Malengo

Lengo ni kuonesha jitihada mbalimbali za Serikali Mtandao zilizofanyika, zinazoendelea na zilizopangwa kufanyika ndani ya Serikali, changamoto na fursa zilizopo na kuzitatua. Katika kikao hicho wadau wa serikali mtandao walibadilishana uzoefu, kujadili njia mbalimbali za kutatua changamoto na kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu serikali mtandao.

Wazungumzaji Wakuu

Wadhamini