Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) inafanya kazi kubwa kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinapatikana kidijitali kwa kutumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA.
Lengo la Sheria ya Serikali Mtandao ni kuhakikisha kwamba Serikali inapata thamani halisi kwenye uwekezaji wa TEHAMA kwa kuwa na utendaji kazi Serikalini ulioboreshwa, utoaji huduma bora kwa umma zinazopatikana kwa urahisi, haraka na kwa gharama nafuu mahali popote na kwa wakati wowote bila kufika ofisi husika.
Mfumo wa Bunge mtandao umesaidia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniawakati wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu (Covid-19) kwa kuepuka kusambaa kwa virusi vya CORONA kwa wabunge na watumishi wa Bunge.
Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-Office) unaongeza ufanisi wa kazi na kupunguza matumizi ya karatasi TPA, NHIF, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano na Ofisi ya Rais - Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
NHIF, DUWASA, TALIRI na MCT zanufaika na matumizi ya mfumo wa mGov unaorahisisha mawasiliano na wadau wa karibu wa Taasisi hizo kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi (SMS).