emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu

-

Kwa niaba ya Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ninayo furaha kuwakaribisha kwenye tovuti yetu mpya pamoja na e-GA TV ambazo kwa pamoja zimeboreshwa na kutengenezwa kwa umahiri mkubwa kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu shughuli zinazofanywa na Mamlaka ya Serikali Mtandao hususani katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma kwa umma kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Ni imani yangu kuwa tovuti hii pamoja na eGA TV (ambayo pia inapatikana kupitia tovuti hii), vitakuwa ni nyenzo sahihi zitakazoiwezesha jamii kupata habari pamoja na elimu kupitia nyaraka mbalimbali na video ambazo zinapatikana kwa urahisi. Nyaraka hizo ni pamoja na Sheria ya Serikali Mtandao ya Mwaka 2019, Kanuni za Serikali Mtandao za mwaka 2020, Miongozo ya Serikali Mtandao ya mwaka 2017, Miongozo ya Kiufundi kwa Mifumo ya Mikutano kwa njia ya Video Serikalini, Ripoti za Utendaji wa Mamlaka. Aidha, tovuti hii ina video mbalimbali kwa ajili ya umma na hivyo kuifanya kuwa ni miongoni mwa sehemu muhimu za marejeo katika masuala mbalimbali ya utekelezaji wa serikali mtandao.

Matumizi ya TEHAMA hutoa matokeo mazuri kutokana na kuboresha utoaji huduma kwa watumishi wa umma na wananchi kwa jumla kwa kutumia miundombinu ya TEHAMA inayosimamiwa kwa weledi ili kufikia lengo la uchumi wa viwanda.

Aidha, napenda kutaja mchango mkubwa na muhimu unaotokana na juhudi endelevu na itikadi yetu katika ubunifu na uboreshaji wa jitahada mbalimbali za serikali mtandao zinazokidhi viwango vya hali ya juu vya kiutendaji vinavyoifanya Mamlaka ya Serikali Mtandao kuwa taasisi ya mfano inayofanya shughuli zake za kila siku kwa kasi na ari inayokubalika. Jitihada hizi na nyingine ni matokeo ya uadilifu mkubwa wa menejimenti na watumishi waliodhamiria kuweka juhudi kubwa katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji huduma bora kwa umma.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu, natoa wito kwa wadau wote kuendelea kuvinjari tovuti hii na e-GA TV mara kwa mara na kuwasihi kuwasiliana nasi kwa na maoni, ushauri kwa ajili ya uboreshaji au kuhitaji ufafanuzi zaidi juu ya huduma zetu.

Tunawakushukuru kwa kuendelea kutuunga mkono na pia bado tuna ari kubwa ya kuendelea kushirikiana nanyi kwa ukaribu zaidi.

Eng. Benedict Benny Ndomba

Mkurugenzi Mkuu