Guidelines for the Management, Operation, and Maintenance of Government Internet Bandwidth in Tanzania Mainland
Mwongozo huainisha seti ya mapendekezo ya taratibu za usimamizi ambao viwango na miongozo inayohusiana na serikali mtandao hupitia kutoka ngazi ya taifa na kuchukuliwa na kutekelezwa ngazi ya taasisi ya umma.
Hutoa maelezo ya usanifishaji utangamanishi kwa namna kuwa program tumizi mbalimbali za taasisi za umma zinatangamanishwa kuwezesha ubadilishanaji taarifa ndani ya serikali.
Inatoa maelezo yanayohusiana na serikali nzima, huduma za serikali, data, program tumizi na modeli rejea za teknolojia zinafafanuliwa.
Hutoa taarifa ya namna ya kukinga na kulinda kiiktisadi taasisi za umma kutokana na matishio ya kiusalama wakati huo huo na kufuata masharti ya kiusalama na kisheria kwa ajili ya usiri, faragha, ufikiwaji, upatikanaji na uadilifu.
Hutoa taarifa kwa serikali kuhusu kubadilishana, kushirikiana na kujumuisha taarifa na kupanga michakato yake kwa kutumia viwango vya wazi vya kawaida
Hutoa taarifa za miundombinu ya teknolojia inayosaidia shughuli za Serikali kama vile seva, kituo cha kazi, uhifadhi na miundombinu ya mtandao, utoaji leseni wa program za kompyuta, kukabili majanga ya TEHAMA na uendelevu wa shughuli, usimamizi wa mtoa huduma za TEHAMA, vipengele vya usimamizi wa rasilimali watu na huduma.
Hufafanua maagizo ya usanifishaji wa taarifa kwa ajili ya ukusanyaji wa data, upatikanaji, umiliki, usalama na usiri, uhifadhi na utunzaji, ufafanuzi na viwango vya matumizi ya data za kawaida na metadata.
Hutoa maelezo yanayohusiana na utoaji wa huduma za Serikali zilizo muhimu, nyumbufu na nyeti kwa mahitaji ya wananchi pamoja na huduma za kawaida zinazoweza kutumiwa tena na taasisi nyingine za umma.
Hutoa taarifa kuhusu usanifishaji mfumo tumizi katika Serikali. Usanifishaji huu unajumuisha maeneo ya utumikaji na urahisi, yanayolenga huduma, uzingatiaji wa viwango vya wazi, utumikaji tena, urahisi wa kubadilika kulingana na hali na kutumika maeneo mengine mbalimabali