OBED MAKOMBE: MFANYAKAZI BORA e-GA 2024/2025

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), imemtangaza Afisa TEHAMA Bw. Obed Makombe kuwa mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2024/2025 huku uwajibikaji na weledi vikitajwa kuwa msingi mkuu wa ushindi huo.Uchaguzi wa mfanyakazi bora wa Mamlaka ulifanyika Februari 26, mwaka huu, baada ya kuwashindanisha wafanyakazi bora 10 kutoka katika idara na vitengo, na kisha Menejimenti kupiga kura ili kumpata mfanyakazi bora wa Mamlaka kwa mwaka wa fedha...