emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Maswali ya Jumla

  1. Ni lazima usajiliwe kwanza kabla ya kuanza kuingia
  2. Upande wa kushoto chini ya Menyu ya TEHAMA, chagua “Security Incident”
  3. Jaza maeneo yote yanayotakiwa kwa mujibu wa fomu
  4. Bofya kitufe cha “Submit” baada ya kukamilisha
  5. Baada ya kufanikiwa kuwasilisha tukio la usalama, utapokea uthibitisho kuwa umefanikiwa kuwasilisha tukio la usalama
  1. Kama huna akaunti ya huduma kwa mteja, tuma baruapepe kwa egov.helpdesk@ega.go.tz au piga simu +255764292299, +255763292299 kuomba akaunti. Akaunti itafunguliwa kwa watumiaji wa taasisi za umma walioidhinishwa tu. Baruapepe ya kuhakiki itatumwa na kukutaka kutayarisha na kuthibitisha nywila yako
  2. Kama una akaunti ya huduma kwa mteja, tuma baruapepe au piga simu +255764292299, +255763292299 kueleza tatizo unalokabiliana nalo
  1. Ni lazima ulingie/logia kwenye GISP kwa kubofya kitufe cha “login” upande a juu wa ukurasa
  2. Ingiza utambulisho wako (jina la mtumiaji na nywila)
  3. Upande wa kushoto kwenye Menyu ya Huduma, chagua “Requested Services”
  4. Huduma zilizoombwa zitaonekana, halafu tafuta au chagua huduma iliyoombwa kuangalia hatua iliyofikia

Huduma na Mifumo ya Mamlaka imepanwa katika makundi yafuatayo;

  1. Huduma za Ushauri wa Kitaalamu na Msaada wa Kiufundi
  2. Mifumo Shirikishi ya TEHAMA
  3. Huduma ya Kuhifadhi Mifumo (Miundombinu kama Huduma , Mfumo kama Huduma)
  4. Utengenezaji Mfumo
  5. Mtandao wa Mawasiliano Serikalini (GOVNET)
  6. Huduma za Serikali kupitia Simu za Mkononi
  7. Utafiti na Mafunzo
  8. Bango la Matangazo
  1. Lazima uingie/logia kwenye GISP kwa kubofya kitufe cha “login” upande wa juu wa ukurasa
  2. Ingiza utambulisho wako jina la mtumiaji na nywila)
  3. Upande wa kushoto kwenye Menyu ya Mradi wa TEHAMA, chagua “Project List”
  4. Orodha ya Miradi itajitokeza, halafu tafuta au chagua mradi ili uone hatua iliyofikia
  1. Bofya linki ya kuingia/logia upande wa juu wa ukurasa
  2. Ingiza utambulisho wako (jina la mtumiaji na nywila)
  3. Unaweza kupata wasifu wa taasisi yako kwa kubofya kitufe cha “institution profile” upande wa juu wa “tab”. Halafu bofya kitufe cha “edit” kuhariri wasifu wako halafu “ save”

TSMS

GISP

GMS