Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), napenda kuwakaribisha katika ukurasa rasmi wa tovuti yetu, ili muweze kupata taarifa muhimu kuhusu majukumu, huduma na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka.
Mamlaka ya Serikali Mtandao, imejizatiti katika kuratibu, kusimamia, na kukuza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Serikalini, ili kuboresha utendaji kazi, utoaji wa huduma bora kwa umma, kuongeza uwazi na kupunguza urasimu kupitia mifumo ya kidijitali.
Mamlaka inaahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Serikali Mtandao kutoka katika Sekta mbalimbali za umma na binafsi, ili kuhakikisha Serikali Mtandao inazidi kuimarika na kuleta tija inayokusudiwa.
Mamlaka imeweza kufikia malengo iliyojiwekea kutokana na utayari wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uwekezaji kwenye Sekta ya TEHAMA.
Mamlaka imedhamiria kuimarisha usalama na udhibiti wa Mifumo ya Serikali, kuimarisha shughuli za utafiti na ubunifu katika utekelezaji wa Serikali Mtandao, kuboresha miundombinu na mifumo shirikishi ya TEHAMA ili kuongeza na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma kidijitali.
Nihitimishe kwa kuwashukuru tena kwa kutembelea tovuti hii, ili muweze kufahamu mambo mbalimbali yanayoigusa taasisi yetu, pamoja na kutoa maoni na mapendekezo kuhusu huduma tunazozitoa.
Karibu tuijenge Serikali Kidijitali

.....
.....
.....
.....
.....
.....
.....
.....