emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

HONGERA e-GA KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MATUMIZI YA TEHEMA SERIKALINI


HONGERA e-GA KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MATUMIZI YA TEHEMA SERIKALINI


Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Kundo A. Mathew (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kazi nzuri ya kuendelea kusimamia na kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahahi na salama ya TEHAMA ndani ya taasisi zote za umma.

Hayo aliyasema wakati wa Kongamano la Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na miaka 10 ya Ndaki ya TEHAMA (CoICT) iliyofanyika Septemba 23, 2022 katika viwanja vya ndaki hiyo Kijitonyama jijini Dar Es Salaam.

“Nachukua fursa hii kuipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuziunganisha taasisi zote za umma kwa kuhakikisha kunakuwepo na matumizi sahihi na salama ya TEHAMA ndani ya taasisi za umma na nazidi kuiomba e-GA iendelee kuziunganisha na kuzisimamia vyema taasisi ambazo bado zipo nyuma kwenye masuala mazima ya TEHAMA” amesema Mh. Mathew.

Aidha, Rais wa Ndaki ya TEHAMA ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam Prof. Joel S. Mtebe ameishukuru e-GA kwa ushirikiano mzuri inayoipatia ndaki hiyo hususani kwenye masuala yote ya TEHAMA katika jitihada za utekelezaji wa Serikali Mtandao.

Prof. Mtebe anasema kuwa Mamlaka hii imekua msaada mkubwa sana kwetu kwenye kutoa ushauri wa mambo mbalimbali yahusuyo TEHAMA pamoja na kutupatia msaada wa kiufundi kwa wakati kila mara inapohitajika.

Katika Kongamano hilo la Miaka 60 ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na miaka 10 ya Ndaki ya TEHAMA, Mamlaka ilipata tuzo ya udhamini iliyopokelewa na Mkurugenzi wa Miundombinu na Uwezeshaji wa Mamlaka Bw. Benjamin Dotto kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka.