emblem
Mamlaka ya Serikali Mtandao
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO/IEC 27001:2022 | ISO 9001: 2015
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Mamlaka ya Serikali Mtandao imefanya kikao chake cha nne (4) cha Baraza la Wafanyakazi tarehe 2 Aprili 2026, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujadili na kupitisha rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Baraza hilo lilifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, inayozielekeza taasisi za umma kuwasilisha na kupata idhini ya bajeti zao kupitia mabaraza ya wafanyakazi, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uwazi na ushirikishwaji katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Katika Baraza hilo, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao Mha. Benedict Ndomba aliwaomba wajumbe kuchangia maoni na kutoa mependekezo yatakayosaidia kuboresha utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.

“Nitoe rai kwa wajumbe kuchangia na kutoa maoni katika kuhakikisha kuwa bajeti inayopitishwa inazingatia mahitaji halisi ya utekezaji wa majukumu ya Mamlaka” Alisema Mha. Ndomba

Katika Baraza hilo, wajumbe walijadili kwa kina vipaumbele vya maendeleo vya Mamlaka, pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida, na bajeti ya miradi ya maendeleo inayotarajiwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Majadiliano hayo yalilenga kuhakikisha kuwa mipango ya taasisi inaendana na malengo yake ya kimkakati, huku ikizingatia matumizi bora na yenye tija ya rasilimali zilizopo.

Hatua hiyo ni muhimu katika kuimarisha ushirikishwaji wa wafanyakazi katika mchakato wa maamuzi, hususan katika masuala ya mipango na matumizi ya rasilimali, na kuhakikisha kuwa bajeti inayopitishwa inazingatia mahitaji halisi ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi.

Mpangilio