emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Tunaishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kubuni,kusanifu na kuujenga mfumo huu


Tunaishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) kwa kubuni,kusanifu na kuujenga mfumo huu


Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba ameziagiza Mamlaka za Maji nchini kufanya kazi kwa kushirikianana Wizara, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Wadau wengine wanaotumia mfumo wa pamoja wa Ankara za Maji nchini ili kuongeza ufanisi, mapato na kuzuia mianya ya rushwa katika utendaji kazi.

Agizo hilo limetolewa mjini Morogoro wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku 10 ya kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia mfumo huo wa pamoja wenye gharama nafuu na unaozingatia viwango na miongozo ya utengenezaji wa mifumo ya TEHAMA Serikalini.

“Ninaamini baada ya mafunzo haya tunaanza kutumia mfumo huu, hii itaokoa upotevu wa mapato unaoendelea na wengine kuendelea kutumia mifumo ambayo hatuna uhakika na usalama wake na inatumia gharama kubwa za uendeshaji” amesisitiza Mhandisi Nadhifa.

Naye, Meneja wa Huduma za Serikali Kupitia Simu za Mikononi kutokaMamlaka ya Serikali Mtandao Bw. Abdalah Samizi ambaye pia ni msimamizi wa mradi huo amesema utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mfumo umekamilika kwa mafanikio makubwa.

“Tumefanya majaribio katika Mamlaka 5 za Maji na kuhudumia akaunti zaidi ya 18500, maombi mapya ya wateja zaidi ya 7600, mikataba ya maji zaidi ya 1100 na kuhudumia akaunti za mita za malipo ya kabla” amesema Bw. Samizi.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Maji, Kitengo cha TEHAMA Mhandisi Masoud Almas amesema Wizara imeamua kutekeleza mradi huo ili kupunguza na kuondoa changamoto mbalimbali katika matumizi ya mifumo ya awali ambapo kila mamlaka ilikuwa inatumia mfumo wake.

Aidha, amesema utumiaji wa mfumo wa pamoja utazisaidia Mamlaka kuondoa urudufu na kuwezesha mifumo kuwasiliana.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo, Mhasibu wa Mamlaka ya Maji Bariadi Bi. Ngoncho Nyamwala ameipongeza Wizara ya Maji na eGA kwa ubunifu mkubwa wa mfumo huo wa pamoja utakaokuwa mkombozi katika kulinda rasilimali za taasisi sambamba na kuongeza ufanisi katika shughuli za kila siku.

“Mfumo huu ni mzuri na umeunganishwa na mifumo mbalimbali ya Serikali, kwa mantiki hiyo ninapendekeza pia maofisa utumishi nao wapewe mafunzo haya kwa kuwa watakuwa sehemu ya mfumo huu”Alisema Bi. Nyamwala.

Mfumo huo umeunganishwa na mifumo mingine muhimu ya Serikali ikiwamo Mfumo wa Malipo ya Serikali Kielektroni (GePG), Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mfumo wa Baruapepe Serikali (eBarua) na Mfumo wa Huduma Kupitia Simu za Mkononi (mGOV).