Mageuzi ya Kidijitali Serikalini Yaipaisha Tanzania Kimataifa

·Tanzania Yatinga Kundi la Juu la Ukomavu wa TEHAMA Duniani kwa mara ya pili. ·Ripoti ya Benki ya Dunia Yathibitisha Mafanikio ya Mageuzi ya TEHAMA Serikalini Na Mwandishi Wetu Tanzania imeendelea kung’ara kimataifa baada ya Benki ya Dunia (World Bank - WB) kuitaja kuwa miongoni mwa nchi zilizo na ukomavu wa juu wa matumizi ya TEHAMA katika sekta ya umma, hatua inayothibitisha mafanikio ya mageuzi ya kidijitali yanayo...



