Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), inatoa huduma ya kuweka matangazo mbalimbali yanayohusu Taasisi za Umma katika kurasa za mbele za Mfumo wa Baruapepe Serikalini (GMS), Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-Office) na Mfumo Shirikishi wa Kusimamia Shughuli na Rasilimali za Taasisi (ERMS).
Matangazo yanayowekwa katika kurasa hizi ni pamoja na yale yanayohusu mikutano, semina, mafunzo na warsha mbalimbali zinazoandaliwa na taasisi za umma ambapo walengwa wakuu ni watumishi wa umma.