emblem
Mamlaka ya Serikali Mtandao
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
ega Logo
Mifumo na Huduma
ega-svg-tree
Uthibitishaji wa Miradi ya TEHAMA

Mamlaka ya Serikali Mtandao inaratibu, kuendesha na kuhakikisha ufuataji wa Viwango na Taratibu za Serikali Mtandao kwa kuimarisha ufuatiliaji na tathmini ya jitihada za serikali mtandao.

Mamlaka hutathmini Miradi ya TEHAMA na uwekezaji katika taasisi ya Umma kwa kutumia vigezo 11:

  • Ubunifu wa Mradi
  • Uboreshaji wa Utendaji Kazi
  • Umiliki wa Mradi
  • Ushirikishwaji Wadau
  • Uhusiano na Miradi mingine Inayofanana
  • Teknolojia
  • Muda Unaofaa
  • Uendelevu wa Mradi
  • Gharama za Mradi
  • Udhibiti wa Vihatarishi
  • Mengine Mbadala au Yakuzingatiwa

Mamlaka inazitaka taasisi zote za umma kuwasilisha taarifa kamili na sahihi za miradi na mifumo yote ya TEHAMA kupitia Tovuti ya Huduma za TEHAMA Serikalini ijulikanayo kama Government ICT Service Portal (GISP), ili e-GA ifanye mapitio ya miradi hiyo na kutoa ushauri wa kitaalam pamoja na kibali kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Hii itaiwezesha Mamlaka kufanya mapitio ya kiufundi ya miradi na mifumo inayopendekezwa, kutoa mwongozo wa kitaalamu, na kutoa vibali rasmi kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Uthibitishaji wa Miradi ya TEHAMA
Mpangilio