emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

KAMATI YA BODI YA UKAGUZI, VIHATARISHI NA UBORA YA e-GA YAFANYA KIKAO


KAMATI YA BODI YA UKAGUZI, VIHATARISHI NA UBORA YA e-GA YAFANYA KIKAO


Kamati ya Bodi ya Ukaguzi, Vihatarishi na Ubora ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), leo imefanya kikao cha kujadili utendaji kazi wa Vitengo vya Ukaguzi wa Ndani na Kitengo cha Usimamizi wa ubora na Vihatarishi vya TEHAMA kwa kipindi cha Julai - Septemba, 2023. Kamati imeeleza kuridhishwa na utendaji kazi wa vitengo hivyo, kwa kufikia malengo kwa asilimia 100, pamoja na kutekeleza kwa wakati maagizo yanayotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).

Aidha, kamati imewasisitiza viongozi wa vitengo hivyo, kuongeza juhudi katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kufikia malengo ya taasisi kama yalivyoanishwa katika Mpango Mkakati wa Mamlaka wa Mwaka 2021/2022 - 2025/2026. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Kituo cha Utafiti na Ubunifu wa Serikali Mtandao (eGOVRIDC) kilichopo jijini Dodoma, na kupata nafasi ya kutembelea na kujifunza kuhusu miradi na bunifu mbalimbali zinazoendelea katika kituo hicho.