emblem
Mamlaka ya Serikali Mtandao
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali, wametakiwa kutumia mifumo rasmi ya Serikali katika mawasiliano ya kikazi ili kulinda taarifa za Serikali dhidi ya vitendo vya uhalifu mtandaoni.

Wito huo umetolewa April mwaka huu  na Mkurugenzi wa Huduma za TEHAMA wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw. Ricco Boma, wakati akichangia mada kuhusu mabadiliko ya teknolojia katika mawasiliano, kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika mkoani Morogoro.

Alisema kuwa, katika ulimwengu wa sasa taarifa ni hazina muhimu inayopaswa kulindwa hhivyo, Maafisa Habari, ambao ndio wenye jukumu la kuuhabarisha umma kuhusu masuala mbalimbali yanayozihusu taasisi zao, wanapaswa kulinda taarifa za Serikali kwa kutumia mifumo rasmi ya Serikali katika Mawasiliano yao.

Alibainisha kuwa, ikiwa Maafisa hao watatumia mifumo isiyo rasmi katika mawasiliano yao, wanaweza kuhatarisha baadhi ya taarifa za Serikali kuwafikia wasiohusika, na hivyo kuliweka taifa katika hatari za kiusalama katika maeneo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Aidha, aliongeza kuwa, matumizi ya TEHAMA katika mawasiliano yana faida nyingi, ikiwa ni pamoja na habari kuwafikia wananchi kwa wakati, lakini pia yanaweza kuleta athari ikiwa mawasiliano ya taarifa za serikali yatafanyika kupitia mifumo isiyokuwa rasmi.,

"Tunayo mifumo mbalimbali kwa ajili ya mawasiliano Serikalini, kama vile Mfumo wa baruapepe Serikalini (GMS), hivyo ni lazima tuhakikishe kuwa, mawasiliano yote ya kiofisi tunayafanya kupitia Mfumo huu na si baruapepe binafsi ili kuhakikisha usalama wa taarifa zetu”, alisema Ricco.

Aliitaja mifumo mingine kuwa ni pamoja na Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-Office) na Mfumo wa e-Mrejesho unaowawezesha wananchi kutoa maoni, ushauri, malalamiko au pongezi kwa Serikali na kisha kupata mrejesho kwa wakati.

Mpangilio