emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

​MIUNDOMBINU BORA NA SHIRIKISHI YA TEHAMA NI MUHIMU KATIKA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA


​MIUNDOMBINU BORA NA SHIRIKISHI YA TEHAMA NI MUHIMU KATIKA KUBORESHA UTOAJI WA HUDUMA KWA UMMA


Serikali inaweka Miundombinu salama ya TEHAMA inayoziwezesha Taasisi za Umma kushirikiana katika matumizi ya rasilimali za TEHAMA ili kuondoa urudufu, kupunguza gharama na kuongeza ubora wa huduma zinazotolewa kwa umma, pamoja na kuhakikisha usalama wa mawasiliano.

Miundombinu iliyopo ni pamoja na Mkongo wa Taifa (NICTBB), Mtandao wa Serikali (GovNet), Vituo vya Kitaifa vya Data na Masafa ya Intaneti.

Hayo yameelezwa na Meneja Usimamizi wa Mtandao wa Mawasiliano Bw. Kulwa Kapama alipofanya mahojiano na mwandishi wetu ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Bw. Kapama amesema kuwa, Sheria ya Serikali Mtandao inazitaka na Taasisikuzielekeza Taasisi za Umma zinazohusika na ujenzi wa Miundombinu ya Serikali kama vile barabara, reli na majengo kuhakikisha kuwa zinawekewa mazingira wezeshi, kwa ajili ya kupitisha Miundombinu ya TEHAMA kuanzia wakati wa kuandaa michoro ya ujenzi wa miundombinu hiyo.

Bw. Kapama ameongeza kuwa, Miundombinu ya TEHAMA Serikalini imesaidia kuboresha mawasiliano katika Taasisi za Umma na kurahisisha upatikanaji wa huduma mtandao zinazotolewa na Taasisi hizo.

Aidha, Bw. Kapama amesisitiza kuwa, kupitia Miundombinu hiyo, Taasisi zote za Umma zinaunganishwa kwenye mtandao mmoja wa mawasiliano ambao ni salama na wenye gharama nafuu ili kuziwezesha Taasisi hizo kuwa na mawasiliano ya kielektroni.

Hadi hivi sasa, zaidi ya Taasisi 394 kutoka Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa, hospitali, Taasisi za Elimu ya Juu, Mahakama na Mamlaka za Maji zimeunganishwa katika mtandao wa Mawasiliano (GovNet).

Hali kadhalika, Mamlaka imetoa huduma ya Masafa ya Internet “bandwidth” kwa Taasisi za Umma 554 ili kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii.