emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

MKAGUZI MKUU WA NDANI WA SERIKALI AFUNGUA MAFUNZO YA WAKAGUZI WA NDANI KUHUSU MIFUMO YA TEHAMA


MKAGUZI MKUU WA NDANI WA SERIKALI AFUNGUA MAFUNZO YA WAKAGUZI WA NDANI KUHUSU MIFUMO YA TEHAMA


Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (IAG) Benjamin Mashauri Magai, leo Aprili 22, 2024 amefungua mafunzo ya siku nne ya Wakaguzi wa Ndani wa Taasisi na Mashirika mbalimbali ya Umma yanayofanyika jijini Arusha kuanzia leo.

Mafunzo hayo yanaratibiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali , yanalenga kuwawezesha Wakaguzi wa Ndani kufanya ukaguzi wa miradi ya TEHAMA kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi.