emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUIMARISHA ULINZI WA MIFUMO YA TEHAMA


TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUIMARISHA ULINZI WA MIFUMO YA TEHAMA


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh.Ridhiwani Kikwete, amezitaka taasisi za umma kuimarisha ulinzi wa mifumo ya TEHAMA ili kuondoa utapeli dhidi ya wananchi unaowezakufanywa na watu wenye nia ovu kupitia mifumo hiyo.

Mh.Kikwete ametoa rai hiyo leo tarehe 8 Februari 2024 jijini Arusha wakati akifunga Kikao Kazi cha 4 cha Serikali Mtandao kilichoandaliwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA).