emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Utafiti na Ubunifu Suluhisho kwa Serikali Mtandao


Utafiti na Ubunifu  Suluhisho kwa Serikali Mtandao


Wanafunzi wanaofanya mafunzo kwa vitendo wameaswa kufanya utafiti na kuwa wabunifu katika masuala ya Serikali Mtandao ili kupata mifumo ambayo ni suluhisho la changamoto zilizopo katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 12, 2022 jijini Dodoma wakati Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deogratius Ndejembi alipokuwa akifunga programu ya nne ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwenye Kituo cha Utafiti, Ubunifu na Uendelezaji Serikali Mtandao cha Mamlaka ya Serikali Mtandao (GovRIDC).

Mhe. Ndejembi aliongeza kuwa, muda wa wiki Nane (8) zilizopangwa kwa vijana hao zimekuwa za mafanikio makubwa kwa kuwa amepitishwa katika maeneo ya kufanyia utafiti na ubunifu na kuona kazi nzuri ambazo zimefanyika na kuamini kuwa ujuzi walioupata utasaidia katika kukuza uchumi wa nchi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehakikisha anapambana kuleta mradi wa Digital Tanzania Project- DTP) ambao ni fursa kwa vijana wabunifu na wenye uwezo wa kuja na suluhisho la namna ya kukabiliana na changamoto zautoaji huduma kwa umma ili kufikia uchumi wa kidijitali.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimeti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Cosmas Ngangaji amesema hivi sasa Dunia ipo kwenye kipindi cha nne cha mapinduzi ya viwanda ambacho TEHAMA ni kipaumbele katika kufikia kipindi hicho. Hivyo, wananfunzi hawana budi kutumia fursa waliyoipata kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa umma kwa njia ya TEHAMA.

Vilevile, Mkurugenzi Mkuu wa eGA Eng. Benedict Ndomba amesema Mwaka 2019 Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao ilianzisha kituo hiki ili kuendeleza tafiti, ubunifu na kujengea uwezo vijana wabunifu na wenye vipaji kwenye eneo la TEHAMA hususani katika masuala ya uendelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao.