emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015

Wadau wa usafirishaji nchini, wameshauriwa kubuni mifumo ya TEHAMA inayoendana na mazingira ya kibiashara


Wadau wa usafirishaji nchini, wameshauriwa kubuni mifumo ya TEHAMA inayoendana na mazingira ya kibiashara


Wadau wa usafirishaji nchini, wameshauriwa kubuni mifumo ya TEHAMA inayoendana na mazingira ya kibiashara ili kuleta tija kwenye taasisi zao .

Rai hiyo imetolewa jana na Meneja wa Usimamizi wa Miradi ya TEHAMA kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Bw.Godfrey Masanja, wakati akiwasilisha mada kuhusu Sheria na Huduma za Serikali Mtandao kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa e-GA Mha. Benedict Ndomba, katika Mkutano wa 16 wa Wadau wa Usafirishaji unaofanyika jijini Arusha.

Bw.Masanja alisema kwa sasa dunia inashuhudia ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji wa huduma kwa wananchi, taasisi za usafirishaji hazina budi kusanifu mifumo inayoboresha huduma hizo kulingana na mazingira yaliyopo.

"Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), ipo tayari kushirikiana na taasisi za uchukuzi katika kushauri na kujenga mifumo mbalimbali ya TEHAMA, itakayosaidia kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika sekta ya usafirishaji na kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi", alisema Masanja.

Aliongeza kuwa, e-GA itaendelea kusimamia matumizi ya TEHAMA serikalini kwa kuzingatia Sera, Sheria, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao ili kuhakikisha yanaleta tija kwa taifa na wananchi kwa ujumla.

Mkutano huo umeandaliwa na Wizara ya Uchukuzi umehudhuriwa na Taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za usafirishaji nchini, huku e-GA ikiwa ni miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo.