emblem
Mamlaka ya Serikali Mtandao
TAASISI YENYE VIWANGO VYA ISO 9001: 2015
ega Logo
Habari
ega-svg-tree

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Mchengerwa amezindua mfumo wa kielekroni unaoitwa "Sema na Waziri” Mfumo huu ni maalumu kwa ajili ya kumuwezesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupokea malalamiko, mapendekezo, pongezi au maulizo ya watumishi na wananchi mahali popote na kwa wakati wowote.


Akizindua mfumo huo Juni 28, 2021 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Utumishi lililopo Mji wa Serikali Jijini Dodoma, Mhe. Mchengerwa amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kunatokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa Wizara ya UTUMISHI kuhakikisha inashughulikia na kuyamaliza malalamiko yote ya watumishi ambayo mengine yamedumu kwa muda mrefu.

''Tunazindua mfumo huu ambao utaniwezesha mimi na wasaidizi wangu kuona malalamiko yanayoletwa na watumishi au wananchi na kuyapatia ufumbuzi haraka. Pia kupitia mfumo nitaona aina ya malalamiko, muda wa kuyashughulikia, hatua zilizochukuliwa na kukamilika kwake. Kwa mfumo huu tunaamini malalamiko haya yatapungua au kumaliza kabisa kama Mhe. Rais wetu alivyoagiza'' Alisema Mchengerwa

Aidha, ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kubuni na kutengeneza mfumo huu ambao ni rahisi kuutumia na wenye kumwezesha kupokea malalamiko ya watumishi kutoka sehemu mbalimbali na kisha kutoa majibu akiwa mahali popote.

Mfumo huu unapatikana kwa anuani ya
www.swu.utumishi.go.tz au kwa kupakua Mobile App ya SWU kutoka Play Store. Aidha, kwa watumishi na wananchi wasiokuwa na simu janja wanaweza kubofya *152*00# kwa kuchagua namba 9 kisha namba 2 na kutuma taarifa yeyote.

Mpangilio