WAZIRI KIKWETE AZINDUA BODI MPYA YA e-GA, AKAGUA UJENZI WA JENGO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amezindua Bodi ya Pili ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) tarehe 27 Januari, 2026.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Kikwete alisema kwamba, Serikali inatambua mchango mkubwa wa e-GA katika ujenzi wa Serikali Mtandao na kuitaka bodi hiyo kuisimamia vema e-GA sambamba na kuimarisha ushirikiano na Menejimenti, ili kuhakikisha dira na maono yake yanafikiwa .
Katika hatua nyingine, Mhe. Waziri alipanda miti ya matunda pamoja na kivuli kuzunguka jengo jipya la Mamlaka katika mji wa Serikali Mtumba jijijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kulinda mazingira.



