emblem

Mamlaka ya Serikali Mtandao

Uadilifu na Ubunifu kwa Utoaji Huduma Bora kwa Umma

Waziri Mchengerwa azionya taasisi za umma


Waziri Mchengerwa azionya taasisi za umma


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora Mhe. Mohamed O. Mchengerwa (mb) amezitaka taasisi za umma kuhakikisha kuwa watumishi wa umma walioajiriwa na kuaminiwa na Serikali wanasimamia utekelezaji wa Serikali Mtandao kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Serikali Mtandao zilizopo ili Serikali ipate tija na ufanisi unaotarajiwa ikiwemo kuongeza usalama wa mifumo na taarifa zilizomo.

Hayo aliyasema leo wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Kanda ya Dar es Salaam na kuunganishwa na watumishi e-GA walio Dodoma Makao Makuu ya Mamlaka kwa njia ya video Dodoma.
Aidha, Mheshimiwa Waziri amesisitiza taasisi zote za umma kuwasiliana na Mamlaka kwa ajili ya tathmini, uhakiki na ukaguzi wa uzingatiaji viwango vya ubora kwa mifumo waliyonayo bila ya kujali imetengenezwa lini na nani.

“Kukiuka Sheria ya Serikali Mtandao Na. 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake na hata kufikia hatua ya kujitoa katika matumizi ya mifumo ya Serikali Mtandao ni sawa na kuhujumu uchumi na Maafisa Masuuli watakaofanya hivyo wanaweza kutenguliwa hata nyadhifa zao” alisisitiza Mhe. Mchengerwa